Anayetaka kunisajili amalizane na Yanga - Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2020
Anayetaka kunisajili amalizane na Yanga - Fei Toto

Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' amesema bado ana mkataba na klabu ya Yanga hivyo kwa timu yoyote inayomuhitaji hapa nchini, inapaswa kwenda kumalizana na mabosi wake

Kumekuwa na tetesi kuwa klabu ya Simba imekuwa ikimnyemelea kiungo huyo ambaye Yanga iliwazidi ujanja mwaka juzi walipo-mpora mikononi mwao na kumsajili

Fei Toto amesema mipango aliyonayo ni kwenda kucheza soka nje ya nchi lakini kama kuna timu inamuhitaji hapa nchini yeye atakuwa tayari kujiunga nayo kama Yanga wataamua kumuuza

"Siwezi kusema nimebakiza mkataba wa muda gani, klabu yangu inajua. Kama kuna timu inanihitaji wazungumze na klabu yangu kwanza. Malengo yangu ni kucheza nje ya nchi (Ulaya) lakini kwa sasa nipo Yanga"

"Ikitokea klabu nyingine inanihitaji hapa Tanzania wakubaliane kwanza na Yanga, Kama Yanga watakubali kuniuza basi Mimi nitaenda," amesema Feisal ambaye amejichimbia visiwani Zanzibar akiendelea na mazoezi binafsi

Fei Toto amerejea katika kiwango chake bora sasa akiwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kocha Luc Eymael

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’