Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema ni suala la muda tu klabu ya Yanga itaingia mkataba wa ushirikiano na moja ya klabu kongwe ya ligi kuu ya Hispani 'La Liga' inayowania moja ya nafasi tano za juu kwenye ligi hiyo
Hersi amesema mkataba huo utafungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika idara zote za uendeshaji, program za mazoezi, aina ya vifaa vitakavyotumika mazoezini, ufundishaji pamoja na kitengo cha kusaka vipaji
Aidha ushirikiano huo utatoa nafasi kwa wachezaji wa Yanga kupelekwa Hispania katika Academy za klabu hiyo, kufanya majaribio lakini pia makocha kupatiwa ujuzi
"Ni kweli tumefikia pazuri na moja kati ya timu inayoshiriki ligi kuu nchini Spain (La liga) juu ya kuingia nayo mkataba"
"Kuna faida nyingi tutapata toka kwao ikiwa ni pamoja na kupeleka wachezaji majaribio, kuwakuza kwenye academy zao pia walimu wetu kupata elimu toka ndani ya klabu hiyo," amesema
Hersi ambaye pia husimamia michakato ya usajili inayofanywa na GSM kwa ajili ya Yanga, amesema kila kitu kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji Yanga, kitakamilika kwa awamu lakini mchakato mzima mpaka kukamilika unaweza kuchukua mpaka miaka mitatu