Mlinzi wa kati wa klabu ya Nkana Fc Mussa Mohamedi amefichua kuwepo kwa mazungumzo baina ya Wakala wake na Yanga juu ya uwezekano wa kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria
Nahodha huyo wa Nkana ambaye pia huchezea timu ya Taifa ya Kenya, amesema mkataba wake na Nkana unamalizika mwishoni mwa msimu hivyo yuko tayari kujiunga na timu yoyote itakayotimiza masharti yake ikiwemo klabu yake ya sasa
Wakati beki huyo akifichua mpango uliopo, uongozi wa Yanga umesema michakato yote ya usajili itawekwa hadharani wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa
Yanga imekuwa ikihusishwa na wachezaji kadhaa hasa baada ya wadhamini wa klabu hiyo GSM kutangaza kutenga Tsh Bilioni 1.5 ili kukisuka upya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
ADVERTISE HERE