Watu 480 wathibitika kuambukizwa corona Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2020
Watu 480 wathibitika kuambukizwa corona Tanzania

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya mwenendo wa Ugonjwa wa Corona nchini

Waziri Mkuu amesema kuwa kuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa Watanzania 196 ambapo kati yao; kutoka Bara ni 174, Zanzibar 22 na kufanya jumla ya watu waliopata maambukizi kuwa ni 480.

Aidha,Waziri Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83).

Hali kadhalika vifo 6 vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa wa Corona kufikia 16 hadi sasa.

Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila Kifo kinachotokea hakisababishwi na ugonjwa wa Corona.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’