Bosi kamati ya usajili ataka subira Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2020
Bosi kamati ya usajili ataka subira Yanga

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga Dominic Albanus amesema ni vyema mashabiki wakasubiri dirisha la usajili litakapofunguliwa kufahamu nyota watakaosajiliwa

Kwa siku za karibuni idadi kubwa ya wachezaji wamehusishwa na Yanga

Dominic amesema mpaka sasa Yanga imehusishwa kutaka kuwasajili zaidi ya wachezaji 30 jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani

"Mimi sijui hizi taarifa zinatoka wapi kwa sababu kama timu bado hatujaanza michakato ya usajili kwa sababu dirisha la usajili bado halijafunguliwa," amesema

"Inawezekana kutokana na janga la corona, shughuli zote za michezo zimesitishwa hivyo waandishi wa habari wanalazimika kutengeneza habari"

Dominic ametoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa tetesi kuwa Yanga imeanza mawasiliano na beki wa zamani wa Simba Juuko Murshidi kwa ajili ya kumsajili

"Hatujawahi kuwasiliana na Juuko, kwanza hatufahamu hata alipo. Kwa kweli tunashangaa habari hizi zinatokea wapi?"

Dominic amesema dirisha la usajili litakapofunguliwa watahakikisha wanaunda kikosi imara kwa kufuata mapendekezo ya kocha Luc Eymael

"Tumedhamiria kuunda kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao tuweze kurejesha utamaduni wa kushinda mataji. Mashabiki wetu wawe na subira, tunawahakikishia yajayo yanafurahisha..!"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’