Kocha msomi zaidi nchini, Profesa Mshindo Msolla aliyewahi kuinoa Taifa Stars, amesisitiza kwamba Yanga ina upungufu na kabla ya haijaingia katika Ligi ya Mabingwa wanatakiwa kufumba macho na kuvunja benki kuingia sokoni kutafuta vifaa vya maana haswa kwenye fowadi.
"Yanga ina upungufu mwingi ambao ni lazima waufanyie kazi haraka kabla ya kuingia katika mashindano makubwa anza kuangalia safu yao ya ushambuliaji sasa wanategemea nguvu ya Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa wale Ngoma na Tambwe bado ni majeruhi,"alisema Msolla.
"Majeruhi ya Tambwe na Ngoma na hata yule Thabaan Kamusoko sio kitu kidogo kutokana na umri watakuwa wanahitaji muda mrefu zaidi lakini timu yao inaumia sasa mtazamo wangu ni kwamba kati ya Tambwe au Ngoma wangemuondoa mmoja ili watafute nafasi ya kuingiza mshambuliaji mmoja mwenye makali.
"Wakiweza wanaweza kuwaondoa hata wote kama watakuwa na nguvu ya fedha, lakini kama hawana wangemuondoa mmoja na waingize mmoja mfano wanaweza kumuangalia yule mshambulaiji wa Prisons ya Mbeya Mohamed Rashid amecheza ligi msimu wake wa kwanza lakini angalia ana mabao sita ni mtu anayeonyesha damu yake inachemka kutokana na umri wake mdogo."
Msolla aliongeza: "Katika viungo wa pembeni, tangu kuondoka kwa Simon Msuva bado Yanga inakosa mtu wa aina yake atakayeweza kuwafanya washambuliaji wa kati kufunga zaidi, afadhali yule Pius Buswita anaonekana kuwa na kitu kipya, kuna kazi kubwa anaifanya yenye msaada kwa timu, lakini yule Mwashiuya bado sana, angeuwa na akili iliyotulia hata dhidi ya Singida angeweza kuipatia bao timu yake na kutengeneza mawili.
"Ni vyema wakamtafuta winga mwenye msaada kurudisha kile alichokuwa anakifanya Msuva kuwezesha washambuliaji kuongeza ubunifu wa kufunga zaidi kwa mipira tofauti.
"Ukiangalia wanapoteza sana mipira kuna maeneo wanakosa viongozi angalia katika ulinzi tangu kushuka kwa Cannavaro (Nadir Haroub) bado hawana mtu wa aina hiyo wanatakiwa kusajili beki bora atakayekuwa na makali ya mipira ya juu kisawasawa.
"Hilo pia la kukosa kiongozi pia lipo katika kiungo ni bora hata sasa amekuja huyu Tshishimbi lakini anakosa msaada kwa wenzake."
Kamati ya Utendaji ya Yanga inafikiria kusajili mastraika wawili wapya kwani wamegundua udhaifu kwenye safu hiyo na wataka kufanya hilo kwenye dirisha dogo.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE