Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo amesema changamoto ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza haina uhusiano wowote na yeye kuwa na tatizo na benchi la ufundi
Shikhalo aliyetwaa tuzo mbili mfululizo za kipa bora wa ligi kuu ya Kenya kabla ya kujiunga na Yanga, amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbele ya mlinda lango mzawa Metacha Mnata
Akijibu swali la shabiki wa Yanga aliyetaka kujua nini kimemsibu mpaka haonekani uwanjani, Shikhalo amesema ni nyakati tu zinapita
"Nataka niwahakikishie mashabiki wa Yanga kuwa mimi sina tatizo lolote na benchi la ufundi. Kutokuniona uwanjani naamini ni mpangilio tu, wakati wangu utafika mtaniona," amesema
Shikhalo alisajiliwa Yanga akitarajiwa kuwa mlinda lango namba moja
Hata hivyo amekutana na changamoto ya kuwania namba na Metacha ambaye kabla ya ligi kusimama kutokana na corona, alikuwa katika kiwango bora zaidi