Pamoja na Serikali ya Kenya kupiga marufu watu kutoka nje kwa muda wa siku 21 kutokana na janga la corona, mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo ameendelea kujifua mazoezi binafsi kujiweka sawa
Shikhalo alirejea Kenya kumzika kaka yake aliyefariki wiki chache zilizopita. Ameshindwa kurejea nchini baada ya Kenya kufunga mipaka kutokana na janga la corona

"Huku Kenya tuna masharti makali kutokana na huu ugonjwa wa corona, hakuna kutoka nje lakini tunashukuru tunapata nafasi ya kufanya mazoezi kujiweka sawa," amesema Shikhalo
" Nitahakikisha naendelea kujiweka sawa na kufanya mazoezi ili kiwango changu kisiporomoke na niendelee kuitumikia Yanga nikiwa na furaha na Amani"
Kipa huyo bora ligi kuu ya Kenya kwa misimu miwili mfululizo, alijiunga na Yanga msimu huu akitokea klabu ya Bandari
Amesema anasubiri mambo yakae sawa ili aweze kurejea nchini kuendelea na majukumu yake Yanga