Mshambuliaji wa Yanga David Molinga anaendelea kujifua kujiweka sawa ili kuendeleza mabao yake pale ligi itakaporejea
Molinga ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa amefunga mabao nane
Mcongomani huyo amesema katika mechi 11 zilizobaki kama atapewa nafasi kwenye kila mchezo ataweza kufunga mabao kati ya 7 na 9
Kama atafunga idadi hiyo ya mabao, atamuweka salama Mwinyi Zahera aliyekuwa kocha wa Yanga ambaye aliahidi kuwa kama Mcongomani huyo hatafikisha mabao 15 au zaidi, akatwe mkono
Molinga alitua Yanga msimu huu kwa mkopo akitokea klabu ya Renaissance Fc inayoshiriki ligi kuu ya DR Congo
Tangu kuwasili kwa kocha Luc Eymael, Molinga amekosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza
ADVERTISE HERE