Jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alibandika picha inayomuonyesha akiwa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mh Anthony Mavunde wakijadili jambo mkoani Dodoma
Baadae Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz alifichua kuwa wawili hao wamekamilisha jambo kubwa muhimu kwa mustakabali wa klabu ya Yanga
"Bora tu niseme kulala na kitu kiuhalisia siwezi, Vijana wawili makini kwenye Ujenzi wa jambo zito na Jambo limekamilika ndani ya mji Mkuu wa Tanzania," aliandika Nugaz kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Pamoja na kuwepo kwa changamoto ya janga la corona, Yanga inaendelea na michakato ya ndani katika kukamilisha mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo
Mfumo huo unaenda kuifanya Yanga iendeshwe kisasa zaidi na itakuwa mfano katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati