Maproo wasiocheza timu za Taifa kunyimwa vibali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2020
Maproo wasiocheza timu za Taifa kunyimwa vibali

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesisitiza kuwa vilabu vitakavyosajili wachezaji wa kigeni ni lazima wahakikishe wachezaji hao wana ubora na wanacheza timu za Mataifa wanayotoka

TFF imesema kuwa hawatatoa vibali kwa wachezaji ambao hawatakidhi kigezo hicho

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, Oscar Milambo amesema katika tathmini yao waliyofanya, wamebaini kuna idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni wamesajiliwa nchini lakini uwezo wao ni wa kawaida

"Baadhi ya timu zimetumia fedha nyingi kusajili wachezaji wa kigeni ambao uwezo wao hauwafikii hata baadhi ya nyota wa ndani. Sasa ili kuboresha Ligi yetu, tutaweka kipengele katika kanuni zetu na kukifanyia kazi wakati wa usajili," alisema Milambo

Hivi karibuni Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Michezo na Taifa (BMT) kutunga sheria itakayoweka ukomo wa wachezaji wa kigeni huku kukiwa na uwezekano mkubwa kuwa idadi ya nyota 10 wa kigeni itapunguzwa

Yanga ilishajipanga

Katika usajili utakaofanywa na Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo Luc Eymael aliweka sharti kuwa kipaumbele cha kwanza kwa nyota wa kigeni anayepaswa kusajiliwa na Yanga inapaswa awe anacheza/amecheza timu ya Taifa analotoka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’