Tshishimbi afichua mpango wa Monzizi kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2020
Tshishimbi afichua mpango wa Monzizi kutua Yanga

Hivi karibuni aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Raul Shungu ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa AS Vita, aliwapa 'mchongo' mabosi wake hao wa zamani kumnasa mshambuliaji wa FC Lupopo Mpiana Monzizi ambaye msimu huu amefunga mabao 11 kwenye ligi kuu ya DR Congo akishika nafasi ya pili nyuma ya Jackson Muleka wa TP Mazembe

Upo uwezekano mkubwa nyota huyo akasajiliwa Jangwani kama wadhamini wa Yanga, GSM watamalizana nae

Nahodha wa Yanga Papi Tshishimbi amefichua mawasiliano yake na mshambuliaji huyo aliyebainisha kuwa kama mambo yataenda sawa atatua Jangwani

"Amenipigia juzi tu hapa nimeongea kwa muda wa kutosha tu ameniambia anataka kuja hapa Yanga na sio klabu nyingine sasa kuna mambo alitaka kujua kwanza juu ya timu yetu na nimemweleza amekubali ameniambia anakuja hapa Yanga," Tshishimbi amenukuliwa na Mwanaspoti

"Mpiana ni mshambuliaji bora sana kama atakuja hapa nafikiri tangu niijue Yanga ndio watafurahi kuona kazi ya mshambuliaji halisi anayejua kupambana na kufunga ndio maana anaongoza kule Congo"

Ikumbukwe pia Yanga inafanya jitihada za kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji wake Heritier Makambo ambapo klabu yake ya Horoya AC imeonyesha kuwa tayari kumuuza ikitaka dau linalofikia Tsh Milioni 140

GSM wamesema watamsajili mchezaji yeyote ambaye dau lake ni chini ya Milioni 500, ilimradi awe amependekezwa na kocha Luc Eymael

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’