Fei Toto ataja siri ya kupiga makombora makali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2020
Fei Toto ataja siri ya kupiga makombora makali

Msimu uliopita kiungo fundi wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' alifunga moja ya mabao ya msimu kwenye mchezo dhidi ya Ruv Shooting akiachia kombora kali je ya 18

Lakini pia, kwenye msimu huo, alifunga bao jingine bora kwa mpira wa adhabu katika mchezo dhidi ya KMC

Mabao yote hayo aliyafunga kwa makombora ya nje ya 18

Fei Toto amefichua kuwa uwezo wa kupiga mashuti makali haukuja kwa bahati bali amekuwa akifanya mazoezi ya kupiga mashuti mara kwa mara

Kiungo huyo mnyumbufu amesema kuwa amejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi ya kupiga mashuti mara tatu kwa wiki

"Moja ya mazoezi ambayo huwa napendelea kuyafanya kwa wiki mara tatu ni kupiga mipira nje ya kumi na nane na huwa nafanya hivyo mara kwa mara ili nijiweke Sawa kwenye ufundi wa upigaji wa namna hiyo"

"Mazoezi hayo yanachangiwa kuweka sawa uwezo wangu wa kupiga mashuti. Hii yote ni kujiweka tayari muda wote pindi nafasi ikitokea na niweze kutumia nafasi na nipate magoli ili niweke rekodi ya magoli ya mbali," amesema Fei Toto

Fei Toto yuko visiwani Zanzibar akiendelea na mazoezi binafsi wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na janga la corona

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’