Huyo Nchimbi ligi ikirejea atawanyoosha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2020
Huyo Nchimbi ligi ikirejea atawanyoosha

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi 'Duma' amesema anaendelea kujifua ili kuendeleza makali yake pale ligi itakaporejea

Nchimbi amefichua kuwa anafanya mazoezi mara tatu kwa siku

"Wakati huu kwangu ni muhimu kufanya mazoezi ili kulinda kipaji changu ukizingatia kwamba kazi yangu ni mpira, ninafanya mazoezi mara tatu kwa siku ila ninachukua tahadhari pia"

"Program ya mwalimu inatutaka tufanye zoezi mara moja ila wakati mwingine ninajiongeza kwa kufanya zaidi ili kuwa bora kikubwa ni umakini pamoja na tahadhari," amesema

Nchimbi alitua Yanga usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Azam Fc lakini akicheza Polisi Tanzania kwa mkopo

Tangu atue Yanga amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao

Kabla ya ligi kusimama, Nchimbi ndiye aliyekuwa mshambuliaji chaguo la kwanza kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

Wakati mwingine kocha Luc Eymael humtumia kama winga, kwani ni mchezaji anayeimudu vyema nafasi hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’