Mayay ataka usajili wa mawinga Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Apr 2020
Mayay ataka usajili wa mawinga Yanga

Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga Ally Mayay ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha pamoja na kuboresha safu ya ushambuliaji wa kati, wanasajili washambuliaji mahiri wa pembeni

Mayay ambaye amewahi kuwe mjumbe wa kamati ya ufundi, amesema msimu huu Yanga imekuwa na mapungufu kwa kukosa aina ya washambuliaji wa pembeni waliokuwa nao miaka ya nyuma

"Ukiangalia soka la Yanga mara nyingi wamekuwa wakitumia mawinga kufanya mashambulizi. Tangu alipoondoka Msuva, Yanga haijapata mbadala wake"

"Ni vyema kipindi hiki wakajaribu kusajili mawinga wa kulia na kushoto ambao wana kasi kama ilivyokuwa wakati wa Msuva," amesema

Mayay pia ameshauri usajili uzingatie upande wa walinzi pembeni ili kuwaongezea nguvu waliopo

"Upande wa safu ya ulinzi hakuna matatizo makubwa lakini ni vyema wakaongeza nguvu. Kwani baadhi ya wachezaji kama Kelvini Yondani, Juma Abdul hawana ubora waliokuwa nao miaka minne iliyopita"

"Magolikipa sidhani kama wanahitaji kusajili. Waliopo wanatosha muhimu waongeze umakini tu ili wafanye vizuri zaidi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
2m ago
READ MORE β†’
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
2h ago
READ MORE β†’
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
3h ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
9h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
21h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1d ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1d ago
READ MORE β†’