Winga wa Yanga Erick Kabamba amesema amekuwa akifanya mazoezi kikamilifu ili kuhakikisha anapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza ligi itakaporejea
Kabamba raia wa Zambia alisajiliwa na Yanga mwezi Januari, usajiri wa dirisha dogo akitokea klabu ya Buildcon ya huko Zambia
Hakuwa na mwanzo mzuri tangu asajiliwe na Yanga, mwenyewe ametaja changamoto iliyomfanya asicheze mara kwa mara
"Kwanza nilikuwa na changamoto ya kuzoea mazingira, nlifanya mazoezi zaidi ili kujiongeza ufiti wa mwili kuwa sawa na wachezaji wenzangu ili kushindana nao katika kuwania nafasi jambo ambalo nilianza kufanikiwa"
"Lakini baada ya ligi kusimama kutokana na janga hili la corona limenifanya pia kupata muda zaidi wa kujifua"
"Kimsingi vikwazo vyote ambavyo vilinifanya kushindwa kupata nafasi ya kucheza nimevimaliza na kipindi hiki nipo na kocha ambaye ananisimamia kufanya mazoezi kwa siku mara tatu ili kuwa bora zaidi ya wakati huu" amesema Kabamba
Kabamba amesema atahakikisha anapambana ili aendelee kubaki kwenye kikosi cha Yanga