Msimu wa 2015/16 Yanga ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Juma Abdul alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi, Amis Tambwe akishinda mfungaji bora wa ligi.
Tambwe anasema, msimu ule magoli yake mengi yalitokana na assists za Juma Abdul na hapa anamzungumzia Abdul ni mchezaji wa aina gani.
“Juma Abdul ni mchezaji mzuri sana, anaweza lakini kila kocha huwa na mipango yake. Zahera ni kama hakumuelewa lakini Juma yuko vizuri sana"
"Nilikuwa nikiona Juma Abdul amevuka mstari wa katikati kwenda kwa wapinzani wetu, mimi tayari naanza kutafuta nafasi ya kujiweka najua krosi yake ataiweka wapi na yeye anajua mimi nitakuwa wapi"
"Nilifunga sana kwa krosi za Juma Abdul msimu nilioshinda tuzo ya mfungaji bora wa ligi nikiwa Yanga"
Katika msimu huo, kocha bora alikuwa Hans van Pluijm na mchezaji bora wa kigeni alikuwa Thabani Kamusoko
Tambwe aliondoka na tuzo ya mfungaji bora akitupia kambani mabao 21

Katika msimu huu Abdul amerejea katika makali yake ya kutoa asisti mpaka sasa akiwa ametoa pasi tano za mabao
Ndiye kinara wa kutoa pasi za mabao kwenye kikosi cha Yanga
Abdul amefichua kuwa kiungo Haruna Niyonzima amekuwa na mchango mkubwa kumfanya awe bora
Abdul amesema ujuzi wa kupiga krosi amejifunza kwa Niyonzima maarufu kama Fabregas