Eymael apendekeza waamuzi sita VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2020
Eymael apendekeza waamuzi sita VPL

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amelishauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuboresha Ligi Kuu Tanzania Bara na kuondoa changamoto kibao zilizomo kuanzia msimu ujao kutumia waamuzi sita.

Eymael amesema kuwa maboresho hayo ambayo alishauri ni muhimu na kama yatafuatwa, basi hakutakuwa tena na malalamiko kwa waamuzi wanaocheza ligi hiyo.

Kwanza, kocha huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akikwaruzana na waamuzi akipinga maamuzi hayo, anataka waamuzi kuongezwa ili kuusimamia mchezo vizuri.

Akifafanua kuhusu hilo, kocha huyo ambaye amekwama kwao Ubelgiji alikokwenda kwa mapumziko mafupi kwa ajili ya kuoa na kushindwa kurudi kwa sababu ya janga la corona, alisema waamuzi hao watasaidia kusimamia mchezo vizuri.

Mbali na kuwa na waamuzi sita, pia kocha huyo ameitaka TFF kuwanunulia waamuzi vifaa vya mawasiliano ili kuhakikisha wanakuwa na mawasiliano ya haraka na uhakika bila kupoteza muda.

Alisema toka aanze kuifundisha Yanga kwenye michezo ya ligi hiyo amebaini makosa mengi yanafanywa mara kwa mara na waamuzi na kusababisha vinyongo na taharuki kwa makocha na mashabiki.

Kuhusu waamuzi, Eymael alisema mbali na waamuzi watano uwanjani, ambapo watakaa kila upande wa lango na mmoja wa akiba ili kumsaidia mwamuzi wakati kama kuna tukio hajaliona.

"Kwa michezo mingi waamuzi wamekuwa wakitoa maamuzi ya ovyo na kwa kuwa tunatumia mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili pamoja na mwamuzi wa mezani, "alisema Eymael.

"Napendekeza maboresho ya aina tatu na kama watafanya hivyo basi ligi itakuwa na ushindani, kwanza wanatakiwa kuanza kuwatumia waamuzi sita, na kati yao wawili wasimame nyuma ya goli, watatu ndani ya uwanja na mmoja mwamuzi wa akiba, "

Pia Eymael amependekeza kutengenezwa kwa utaratibu mzuri wa kuweka kumbukumbu za wachezaji na makocha kwa ajili ya kuwapa tuzo kwa wale watakaofanya vizuri.

Utaratibu wa kutumia waamuzi sita umeshawahi kutumika katika mchezo wa Yanga na Simba uliofanyika hivi karibuni, ambapo Yanga walishinda 1-0, na katika mashindano ya kimataifa ya U 17 yaliyofanyika nchini.

HabariLeo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
25m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’