Wakati timu mbalimbali zikichukua hatua za kuwapunguzia wachezaji mishahara baada ya ligi kusimama kutokana na janga la corona, uongozi wa klabu ya Yanga bado haujafikiria kuchukua hatua kama hiyo
Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji wao wameendelea kulipwa mishahara yao kama kawaida licha ya ligi kuwa imesimama
"Sisi hatujafikiria mpango huo, wachezaji wetu wanalipwa mishahara yao kama kawaida," amesema
Aidha Bumbuli amesema kocha Luc Eymael amekuwa akiwapa program mbalimbali za mazoezi ambazo wanafanya majumbani kwao
ADVERTISE HERE