Unamkumbuka yule mshambuliaji wa Rayon Sports ambaye Yanga ilidaiwa kumuwania kwenye usajili wa dirisha dogo?
Anaitwa Michael Sarpong raia wa Ghana, ambaye ni mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo
Hivi karibuni uongozi wa Rayon ulieleza mpango wake wa kusitisha kuwalipa mishahara wachezaji baada ya ligi kusimama kwa muda kutokana na changamoto ya janga la corona
Sarpong ni miongoni mwa wachezaji waliopinga mpango huo ambapo nyota huyo katika mahojiano ya redio moja ya Rwanda alidai Rais wa klabu ya Rayon Munyakazi Sadate ameshindwa kuiongoza timu hiyo
Lakini pia Sarpong alilalamika kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu na wamekuwa na maisha magumu wakati huu ambao wako majumbani mwao tu kujilinda na corona
Taarifa kutoka Rwanda zinadai kuwa Rayon imeamua kuvunja mkataba wake wakidai maneno yake yamemkosea heshima Rais wa klabu hiyo
Msimu huu Sarpong meifungia Rayon mabao 16, baada ya mkataba wake kuvunjwa Sarpong amekuwa mchezaji huru
Pengine hii ni nafasi adimu kwa Yanga kuweza kumnasa mshambuliaji huyo