Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa amesema, hadi Aprili 21, 2020 jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na Virusi vya Corona.
Kati yao, wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumatano April 22, 2020 akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dares salaam
Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na Wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284)
Mara ya mwisho (Jumatatu April 20, 2020) Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa Corona ilikuwa 254 baada ya Wagonjwa 84 kuongezeka
Mapema leo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa mchanganuo wa wagonjwa 30 wapya ambapo Dar es salaam wamepatikana wagonjwa (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani (2), Kagera (1), Dodoma (2), Manyara (1) na Morogoro (1)
Serikali imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo ambao bado ni tishio kwa dunia nzima