Simba imepata ushindi 'tata' wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa leo Jumapili.
Utata wa ushindi huo unatokana na bao alilofunga mshambuliaji wake Shiza Kichuya ambaye licha ya kamera za Azam TV kushindwa kuchukua tukio vizuri, Kichuya alipokea pasi ya Jonas Mkude akiwa eneo la kuotea.
Bila shaka msema chochote wa Simba Haji Manara ataitisha mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa bao hilo kama alivyofanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga.
Simba imefikisha alama 19 na kuiondosha Azam FC kileleni kutokana na wingi wa mabao yake.
Mchezo wa Lipuli FC dhidi ya Mwadui FC umemalizika kwa sare ya bao 1-1.

ADVERTISE HERE