Beki wa kulia wa Yanga Paulo Godfrey 'Boxer' amesema anatumia kipindi hiki cha ligi kusimama kutokana na changamoto ya corona kujiimarisha
Msimu huu hakuwa mzuri sana kwa Boxer kutokana na majeraha ya mara kwa mara yanayomsumbua
Nyota huyo aliyepandishwa kikosi cha kwanza msimu uliopita na aliyekuwa Mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema hali yake imeimarika
"Nimekuwa nikisumbuliwa na majeraha, lakini namshukuru mungu sasa naendelea vuzuri nafanya mazoezi kujiweka fit," amesema
Tangu atue kocha Luc Eymael, Boxer hajaonekana kabisa dimbani, majeraha ikitajwa kuwa sababu
Boxer alipata matatizo ya nyama za paja kwenye mcheza wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Towsnhip Rollers ambao ulipigwa jijini Dar es salaam
Kisha akajitonesha tena kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa huko Botswana
Tangu wakati huo Boxer hakuweza tena kurejea dimbani kutokana na majeraha hayo kutopona sawasawa