Habari njema ni kuwa klabu ya Yanga iko katika nafasi nzuri ya kumsajili beki wa Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto
Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto amekiri kuwepo kwa mazungumzo baina ya klabu yake na uongozi wa Yanga kuhusu beki huyo wa timu ya Taifa
Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Mguto amesema mazungumzo baina yao yamekamilika na hivyo Yanga ina nafasi nzuri ya kumsajili beki huyo kinda mwenye umri wa miaka 22
Inaelezwa Coastal Union imemuweka sokoni Mwamnyeto ikitaka dau la Milioni 100, lakini klabu hiyo iko tayari kwa majadiliano kwa timu yoyote inayomuhitaji
Mwezi Januari Yanga ilijaribu kumsajili Mwamnyeto lakini mpango huo ulikwama baada ya pande mbili kushindwa kufikia makubaliano
Mwamnyeto ana mkataba wa mwaka mmoja umebaki na klabu ya Coastal Union