Ule mchakato wa kulirejesha sokoni Jarida la klabu ya Yanga umekamilika na toleo la kwanza la Jarida hilo litakuwa sokoni hivi karibuni
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki kujiandaa kununua jarida hilo litakalokuwa limesheheni mambo kemkem, litapatikana kwa Tsh 5,000/- tu
Mradi huo uliasisiwa na aliyekuwa Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten ambaye kwa sasa ni Afisa Masoko
Ten alifanikiwa kutoa matoleo mawili kabla ya mradi huo kukwama
Hii ni hatua muhimu kuelekea uzao mpya wa klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE