Winga Saimon Msuva ndiye mchezaji wa mwisho ambaye Yanga inaweza kujivunia kuwa aliitendea haki nafasi yake
Tangu kuondoka kwa nyota huyo, ni dhahiri pengo lake limekuwa gumu kuzibika
Kwani ni nadra sana mshambuliaji wa pembeni kuibuka kuwa mfungaji bora wa ligi, Msuva alifanya hivyo mara mbili
Uongozi wa Yanga unafanya jitihada kuhakikisha msimu ujao ule utamaduni wa kushambulia kupitia pembeni unarudi
Uzuri hata kocha Luc Eymael ni muumini wa soka la aina hiyo ndio maana hata mapendekezo yake ya usajili wa wachezaji wa pembeni wote ni 'viberenge'
Wakati akiwa tayari na Morrison upande wa kushoto, Yanga inasaka winga wa upande wa kulia ambaye atakuwa aina ya Msuva
Tusila Kisinda ndio jina la kwanza ambalo Eymael alipendekeza asajiliwe 'kwa gharama yoyote'
Lakini ikitokea itashindikana kumnasa winga huyo anayechezea AS Vita, Mbelgiji huyo amependekeza kusajiliwa kwa Harrison Mwendwa anayekipiga Kariobang Sharks ya nchni Kenya
Inaelezwa Eymael alimuona nyota huyo kupitia mkanda wa video wa mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi kati ya Yanga dhidi ya Sharks ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1
Hata hivyo Yanga ilijaribu kumsajili Mwendwa wakati wa Zahera lakini ilishindikana kutokana na dau kubwa alilotaka nyota huyo
Kwa upande wa nyota wazawa ambao wanatupiwa jicho ni pamoja na Salum Kihimbwa wa Mtibwa Sugar, Marcel Kaheza wa Polisi Tanzania na Hassa Dilunga wa Simba