Mapema leo baadhi ya wachezaji wa Yanga walitembelea duka la moja ya wadhamini wa klabu hiyo GSM Mall lililoko Mlimani City jijini Dar es salaam
Nyota hao walijipatia mahitaji yao ya vifaa mbalimbali vya michezo ambavyo vitawasaidia wakati huu wakiendelea na mazoezi binafsi kutokana na janga la Corona
Kila mchezaji alipewa vocha ya Tsh laki sita ambayo ndiyo aliyotumia kununua mahitaji yake kwenye maduka ya GSM hapo Mlimani City
Wachezaji ambao wapo nje ya Dar watakutana na Vocha zao wakirejea.


ADVERTISE HERE