Kiungo mshambuliaji wa Yang Benard Morrison amewapa dili mabosi wake kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ghana Mumuni Shafiu, imefahamika
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, anakipiga kunako klabu ya Ashanti Gold
Inaelezwa dili la usajili wa mshambuliaji huyo linasukwa na Morrison ambaye kocha Luc Eymae alimuachia kazi maalum ya kumuweka sawa kabla Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said hajaenda 'kufanya yake'
Katika moja ya mahojiano yake, Eymael alifichua kuwa na mpango wa kusajili mchezaji kutoka Ghana ingawa hakuwa tayari kutaja jina la mchezaji huyo
Aidha, mmoja wa viongozi wa Yanga amekiri kuwepo kwa mpango wa kumnasa mshambuliaji huyo
"Kocha tayari analo jina la mchezaji huyo, kwa sasa anaangalia kama atafaa au la, ingawa jicho la kwanza la Morrison limeshakiri ni kifaa kizuri"
"Kocha mkuu amekuwa akimfuatilia mchezaji huyo anayecheza katika moja ya timu za nchini Ghana na kisha kumshirikisha Morrison ambaye kwa upande wake, amesema asajiliwe bila shaka"
"Hii ina maana kuwa Morrison amepata pacha wake hivyo watasaidiana kuhakikisha Yanga inavuna mabao mengi msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa," alisema