Mfumo wa uwekezaji Yanga utakuwa bora kuliko Simba - Rage

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2020
Mfumo wa uwekezaji Yanga utakuwa bora kuliko Simba - Rage

Licha ya Klabu ya Simba kutangulia kuingia katika mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji, aliyekuwa Rais wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi hao, Ismail Aden Rage, amesema mfumo watakaokuja nao watani zao Yanga utakuwa mzuri na wenye maslahi zaidi kwa wanachama wao

Desemba 3, 2017, Mwenyekiti wa Kamati ya mchakato wa mabadiliko ya Klabu ya Simba, Jaji Mihayo, alimtangaza Mohamed "Mo" Dewji, kuwa mshindi wa zabuni ya uwekezaji baada ya kuweka mezani ofa ya Sh. bilioni 20 akiwa mgombea pekee aliyejitokeza.

Mchakato ambao umefikia hatua nzuri na mabadiliko ya kiuendeshaji katika klabu hiyo yameanza kuonekana huku Mo Dewji kwa sasa akiwa mwekezaji na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, ambako atamiliki asilimia 49 za hisa na 51 zikimilikiwa na wanachama wa Simba.

Hata hivyo, wiki iliyopia, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema kwa sasa Sh. bilioni 20 za mwekezaji huyo bado hazijawekwa katika akaunti ya klabu kwa sababu ya kutokamilika kwa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na kufungua kampuni (Simba Sports Club Limited), jambo ambalo wanaamini litakamilika ndani ya mwaka huu.

Alisema kwa sasa fedha hizo zimewekwa katika akaunti maalumu (fixed account) ya Mo kwa makubaliano yaliyofikiwa na bodi ya wakurugenzi na kila mwezi anatoa kiasi cha Sh. milioni 165 ili kusaidia shughuli za kiutawala za klabu hiyo.

Dalili hiyo ya mafanikio ambayo imefikiwa na Simba, imewaibua watani zao Yanga, ambao walishajaribu kufanya hivyo zaidi ya mara tatu wakashindwa, walipoanza mwaka 1994 kupitia kwa marehemu George Mpondela na Tarimba Abbas.

Lakini, Rage ameibuka na kueleza kuwa mfumo wa uwekezaji wa Yanga utakuwa mzuri zaidi ya huo wa Simba kwa kuwa wao ni wa 'public' (wananchi) ambao utatoa nafasi kwa wanachama kuweza kuuza hisa zao.

"Kwa mfumo wa Simba wenyewe ni 'private' wanachama hawataweza kuuza hisa, kuna kitu kimejifunga katika mfumo huu wa Simba, ndiyo maana nasema wa Yanga utakuwa mzuri zaidi.

"Ndiyo maana Yanga wanajiita timu ya wananchi, mfumo wao ni kama wa chama changu cha CCM kilivyopitia kabla ya kuitwa CCM," alisema.

Rage alisema hata katiba ya Yanga ni nzuri kuliko yao na mara kadhaa amekuwa akisisitiza si mbaya kuiga mazuri yaliyopo ndani ya katiba hiyo.

Yanga ilitangaza hadi kufikia Mei, mwaka huu itanza rasmi mchakato wa uwekezaji kwa kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji, lakini baada ya mlipuko wa virusi vya corona (COVID-19) vilivyosababisha serikali kuzuia shughuli zote za mikusanyiko, uongozi wa klabu hiyo umeeleza ni kikwazo kwao kuweza kuitisha mkutano wa wanachama ili kupata baraka zao na kufanya marekebisho ya katiba.

Nipashe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’