Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Singida United, kikosi cha Yanga kinarejea leo jijini Dar es salaam kuanza maandalizi ya mchezo unaofuatia dhidi ya Mbeya City, Novemba 19.
Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Uhuru, jijini Dar es salaam. Ni baada ya michezo ya kalenda ya FIFA.
Baada ya kupata suluhu dhidi ya Singida United, Yanga inashika nafasi ya pili ikijikusanyia alama 17.
Azam FC iliilaza Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo uliopigwa jana usiku hivyo kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kufikisha alama 19.
Baadae Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City katika moja ya michezo inayotarajiwa kupigwa leo Jumapili.
Msimamp wa ligi unaweza kubadilika kama Simba itashinda au hata kupata sare kwenye mchezo huo.
Ushindi utairudisha Simba kileleni wakati sare itaifanya timu hiyo ishike nafasi ya pili huku Yanga ikishuka nafasi ya tatu.

ADVERTISE HERE