Yikpe aomba apewe muda Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2020
Yikpe aomba apewe muda Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Yikpe Gnamien amesema anatambua ana deni kubwa na klabu hiyo ambayo ilimsajili dirisha dogo mwezi Januari mwaka huu akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Gor Mahia

Tangu atue Yanga, Yikpe amekuwa kwenye wakati mgumu, ni kutokana na mashabiki wengi wa Yanga kutoridhishwa na uwezo wake

Hata hivyo mwenyewe amesema anachohitaji ni muda tu kuweza kuwafurahisha

Yikpe amesema anafahamu nini mashabiki wanataka, jambo linalomfanya ajihisi kuwa na deni kubwa

"Nina mkataba na klabu yangu na natamani kuifanyia makubwa. Nahisi nina deni kubwa kwa klabu na mashabiki," amesema

"Ligi ikianza natamani kulipa madeni hayo. Sifikirii kuondoka Yanga wakati huu kwani ukiondoka sehemu kabla ya kuonesha uwezo halisi huko uendako kuaminiwa ni ngumu. Nahitaji muda zaidi na Yanga," amesema

Yikpe amefunga mabao mawili tangu atue Yanga. Bado hajaonyesha makali yanayoweza kuwashawishi mashabiki wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’