Huyu Kabwili amekosa nafasi tu Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
20 Apr 2020
Huyu Kabwili amekosa nafasi tu Yanga

Zipo taarifa kuwa miongoni mwa nafasi ambazo kocha Luc Eymael amependekeza usajili mpya ni nafasi ya mlinda lango

Kwa sasa Yanga ina walinda lango watatu, Metacha Mnata, Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili

Farouk na Metacha ndio wamepata nafasi zaidi msimu huu wakati Kabwili hakupata nafasi ya kucheza mechi yoyote ya kimashindano

Lakini msimu uliopita Kabwili ndio alikuwa kipa tegemeo hasa baada ya Beno kufanya mgomo

Pengine msimu huu hakupata nafasi ya kudhihirisha ubora wake, Yanga inaweza kufanya makosa kama wataamua kumuacha

Kabwili umri wake bado ni mdogo, ana muda mrefu wa kusakata kabumbu

Alijiunga na Yanga akiwa na umri wa miaka 17 tu na ameingia kwenye rekodi ya CAF ya mchezaji mdogo zaidi kucheza  michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, akidaka mchezo dhidi ya Township Rollers mwaka juzi

Kabwili bado ni miongoni mwa makipa bora Tanzania, changamoto ya kukosa nafasi ndio inamfanya asionekane

Pengine ligi itakaporejea, kwenye mechi zilizobaki ni vyema mlinda lango huyo akapewa nafasi ya kukaa langoni katika mechi kadhaa

Naamini kama Eymael atamshuhudia Kabwili katika mechi tatu tu, atafuta mpango wake wa kusaka mlinda lango mwingine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’