Pluijm aikumbuka Yanga yake ya mwaka 2016

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2020
Pluijm aikumbuka Yanga yake ya mwaka 2016

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga kwa vipindi viwili tofauti, Hans van Pluijm amesema katika maisha yake ya ukocha hataisahau timu ya Yanga aliyokuw anayo msimu wa 2015/16

Pluijm aliisaidia Yanga kutwaa mataji mawili mfululizo ya ligi kuu msimu wa 2014-15 na 2015/16 kabla ya kumuachia George Lwandamina ambaye alimalizia nusu ya msimu wa 2016-17na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa tatu

Pluijm amesema kikosi alichokuwa nacho 2015/16 ndio kikosi bora zaidi ambacho anasema mpaka sasa Yanga imeshindwa kupata timu kama ile

Katika msimu huo, Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Pluijm ametamba kikosi chake cha msimu huo kilikuwa na mafundi kwelikweli hivyo kumfanya asiwe na kazi ngumu kwenye benchi

"Sikuwa na kazi kubwa ya kufanya kwa sababu nilikuwa na wachezaji wenye kushika kwa haraka maelekezo. Nilikuwa na Niyonzima, Kamusoko kati kati walikuwa wakicheza kwa spindi na kupiga pasi nyingi za mbele," Pluijm amenukuliwa na Mwanaspoti

"Kuna muda ilibidi wacheze wote, Tambwe na Ngoma kwa sababu nilikuwa nikipata tabu kufanya uchaguzi, kila mmoja alikuwa na soka lake tofauti na walijua kufunga, mmoja alikuwa akiumia sikuwa na hofu ya kubaki na mshambuliaji mmoja kwa sababu waliliokuwa wakicheza pembeni nao waliweza kufunga"

Pluijm aliisaidia timu hiyo kubeba mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara (Vpl), Ngao za hisani mara mbili na Kombe la FA mara moja.

Mwaka 2016, Hans aliamini walikuwa na uwezo wa kufika hata hatua ya nusu fainali ambayo viongozi wa Yanga yalikuwa matamanio yao baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika Ligi na michezo ya awali hadi kutinga hatua hiyo.

Yanga ya wakati huo iliundwa walinda lango, Ally Mustafa, Deo Munishi na Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Andrew Vincent, Nadir Haroub, Vicent Bossue, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Oscar Joshua na Juma Abdul

Viungo na washambuliaji, Juma Makapu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima na Donald Ngoma

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
59m ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’