Kocha wa zamani wa Yanga Raul Shungu amewashauri mabosi wake hao wa zamani kumsajili mtupia mabao wa FC Lupopo Mpiana Monzinzi
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, msimu huu amefunga mabao 11 akishika nafasi ya pili katika vita kuwania kiatu cha dhahabu akichuana vikali na Jackson Muleka wa TP Mazembe aliyefunga mabao 12
Shungu ambaye ni kocha msaidizi wa AS Vita amesema, mshambuliaji huyo anaweza kuwafaa Yanga katika jitihada zao za kurejesha makali ya kikosi chao
"Monzinzi ni mchezaji mzuri, amekuwa na msimu mzuri Lupopo, kama Yanga watamsajili wanaweza kunufaika nae," amesema Shungu ambaye inaelezwa Yanga inamtumia katika jitihada zao za kumnasa winga wa AS Vita Tusila Kisinda"
FC Lupopo inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu ya Congo maarufu Linafoot. Timu hiyo imefunga mabao 23 ambapo kati ya mabao hayo, Monzinzi amefunga mabao 11 ambayo ni karibu nusu ya mabao yote
Nyota huyo anatajwa kuwaniwa na vilabu kadhaa huko Congo ingawa hapa Tanzania, klabu ya Simba inatajwa kumuwania pia