Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Sheria, Hadhi ya Wachezaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alex Mgongolwa, amewataka wachezaji kuwa makini katika suala zima la kusaini mikataba na viongozi wa klabu mbalimbali.
Kauli hiyo ya Mgongolwa imekuja wakati wachezaji kadhaa wakiwa katika mazungumzo na viongozi wao ili kuongeza mikataba yao
Mgongolwa amesema ili mchezaji awe salama katika mkataba na klabu anayoingia nayo mkataba lazima awe na wanasheria wa kuwasimamia.
Amesema wachezaji wengi wanajikuta wanaingia katika migogoro na klabu zao kuhusu mikataba kwa sababu hawana wanasheria.
"Wachezaji wa Tanzania wanatakiwa kubadilika na wafanye kazi kwa uweledi, yale masuala ya kuingia mkataba kizembe umepitwa na wakati"
"Unamkuta mchezaji hajui hata mkataba unatakiwa kuwa na vitu gani yeye anasaini tu kwa sababu kaambiwa anapewa fedha nyingi na mwisho wa siku kile walichozungumza kwa mdomo na kilichopo katika maandishi ni vitu viwili tofauti na ndio sababu ya kuanza kuleta mzozo baina yao," asema Mgongolwa.
Amesema kutokana na kuwapo wa kesi nyingi za mikataba kati ya mchezaji na viogozi wa klabu, umefika wakati wa wachezaji kuwatumia wanasheria katika kuwasimamia masuala yao ya soka