Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa amejichimbia wilayani Bagamoyo kunoa makali wakati huu ligi ikiwa imesimama kutokana na janga la corona
Baada ya kumaliza mapumziko yake mkoani Mwanza, moja kwa moja Ngasa alielekea Bagamoyo ambako amesema ameweka kambi kunoa makali yake
Mkongwe huyo anaamini ligi itakaporejea atakuwa na mchango kuisaidia timu yake kutimiza malengo yaliyowekwa ambayo ni kumaliza katika nafasi za juu ligi kuu ya Vodacom pamoja na kutwaa taji la FA
"Kwa sasa niko Bagamoyo, nimetafuta sehemu nzuri yenye utulivu kwa ajili ya kufanya mazoezi, nafanya hivi ili kulinda kipaji changu, nikimaliza programu ya kujifua, ninapata pia muda wa kupumzika," alisema Ngasa.
Aidha, Ngasa hakuacha kumtupia 'dongo' swahiba wake Deus Kaseke akimtaka arudi jijini Dar es salaam kujifua
"Namshangaa Kaseke (Deus), bado yupo Mbeya, anatakiwa kurudi mjini na kuendelea kujifua, huu si muda tena wa kushangaa"