Yanga yaongeza masharti usajili nyota wa kigeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2020
Yanga yaongeza masharti usajili nyota wa kigeni

Katika kuhakikisha wanasajili wachezaji wa kigeni ambao watakuwa na uhakika wa kuisaidia timu kufikia malengo yake, kipaumbele cha kwanza kwa mchezaji anayepaswa kusajiliwa na Yanga ni lazima awe anacheza timu ya Taifa, imefahamika

Yanga pia imeweka mkazo kwa kigezo hicho ili kwendana na matakwa ya Shirikisho la soka nchini (TFF) ambalo inaelezwa kuanzia msimu ujao litavibana vilabu kuhakikisha vinasajili wachezaji wa kigeni ambao wana hadhi na wanacheza timu za Taifa

Lakini pia Yanga haitasajili mchezaji ambaye katika timu aliyokuwa akicheza hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Kigezo hicho pia inaelezwa kitawahusu wachezaji wazawa ambao wanawaniwa na timu hiyo

Mmoja wa viongozi waandamizi wa Yanga amesema wanafahamu kusajili wachezaji wa kigeni ambao wanacheza timu za Taifa itawagharimu fedha zaidi lakini wadhamini wao kampuni ya GSM wamewaruhusu kutekeleza mpango huo

"Msimu huu tumepata hasara kwa kusajili wachezaji wengi wa kigeni kiholela. Hatutarudia makosa ndio maana tumeongeza umakini kwenye usajili unaokuja.. Ni bora tutumie Milioni 300 kusajili mchezaji mmoja mzuri kuliko kusajili wachezaji watano ambao hawana mchango mkubwa kwa timu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’