Mlinzi wa pembeni wa mabingwa soka Tanzania Bara, Yanga Juma Abdul bado mkataba wake haujamalizika, ni mwaka mmoja umesalia ili mktaba wake umalizike.
Baadhi ya magazeti yamekuwa yakipotosha kudai Abdul anataka kuondoka Yanga. Mwenyewe amekanusha upotoshaji huo.
Swala lake limekuwa likipotoshwa sana kama lilivyo swala la Simon Msuva ambaye mwenyewe amekiri kuwa mkataba wake na Yanga bado uko hai mpaka mwishoni mwa msimu ujao(imesalia miezi 10).
Katika wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Haruna Niyonzima na Vicent Bossou pekee ambao kocha aliwahitaji lakini klabu imeshindwa kufikia nao makubaliano.
Wengine wote waliokuwa kikosi cha Yanga msimu uliopita wataendelea kubaki Jangwani isipokuwa wachache ambao Yanga imewapa nafasi ya kuangalia pahali pengine.
Uongozi wa Yanga utaweka hadharani kikosi cha msimu ujao wakati wowote kwani klabu inatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya Julai 04, 2017.

ADVERTISE HERE