Inaelezwa klabu ya Yanga ina uhakika wa kuipata saini ya kiungo mkabaji wa Rayon Sports na timu ya Taifa ya Rwanda Ally Niyonzima
Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakifuatiliwa na kocha Luc Eymael kuwaongeza kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, ana uzoefu wa soka la ushindani kwani amepata nafasi ya kushiriki mechi za Kimataifa akiwa na Amavubi, Al Bashaer ya Oman, AS Kigali na Sofapaka ya Kenya
Inaelezwa kiungo Haruna Niyonzima anaweza kuwa amehusika kumshawishi mwamba huyo anayecheza nae timu ya Taifa
"Mazungumzo yamekamilika, mambo yakiwa sawa Niyonzima anaweza kusaini mkataba wa miaka mitatu," kilisema chanzo
Nafasi ya kiungo mkabaji ni moja ya nafasi ambazo Eymael ametaka iongezewe nguvu
Eymael amekuwa akimtegemea zaidi Tshishimbi kwenye nafasi hiyo licha ya kuwa na mzawa Abdulaziz Makame 'Bui' anayeonekana kutomshawishi Mbelgiji huyo
Ujio wa kiungo huyo huenda ukamuweka kwenye mazingira magumu zaidi Bui kuendelea kubaki Yanga