Mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga unaendelea licha ya changamoto ya janga la corona
Pengine kama sio janga hili, mchakato huo tayari ungekuwa hadharani
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema wadhamini wao, GSM wametenga Dola laki nne (karibu Tsh Bilioni 1) kuhakikisha mchakato huo unakamilika
GSM wametoa fedha hizo kama wadau wa Yanga ili kusimamia hatua za awali za mchakato huo
Nugaz amesema fedha hizo zitatumika katika kuwalipa wataalam kutoka Barani Ulaya na Afrika ambao wanasimamia mchakato huo katika awamu ya kwanza itakayochukua takribani miezi sita
Baadae jukumu hilo litaachwa mikononi mwa klabu ya Yanga yenyewe
Juzi Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alifichua kuwa Yanga itasaini mkataba wa ushirikiano na ligi kuu ya Hispania (La Liga) pamoja na klabu kongwe inayoshiriki ligi hiyo ambayo inaelezwa Yanga itatumia mfumo unaotumiwa na klabu hiyo