Yanga yasaka washambuliaji kila pembe ya Afrika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Apr 2020
Yanga yasaka washambuliaji kila pembe ya Afrika

Wakati hatma ya ligi kuu ikiwa bado inasubiri kumalizika kwa changamoto ya ugonjwa wa corona, huko Jangwani tetesi za usajili zimeendelea kushika kasi

Iko hivi, Yanga imepania kufanya usajili mkubwa ambapo GSM, wadhamini/wahisani wameapa kuunda kikosi cha maangamizi ambacho kitamponda kila atakayekuja mbele ya Yanga msimu ujao hesabu zikiwa kurejesha ubingwa walioupoteza kwa msimu wa tatu sasa

Safu ya ushambuliaji ndio inayowafanya mabosi wa Yanga wawe 'busy' kusaka nyota wenye uwezo mkubwa kwani msimu huu mambo hayajawa sawa sana kwa upande wa ushambuliaji

GSM imetenga kitita cha zaidi ya Bilioni 1.5 ambapo inaelezwa zaidi ya nusu ya fedha hizo itaelekezwa kuimarisha safu ya ushambuliaji

Mcongomani Heritier Makambo ni nyota wa kigeni wa kwanza ambaye GSM wameahidi watamvalisha uzi wa njano na kijani msimu ujao

Lakini pia inaelezwa kuwa mabosi wa GSM wanaweza kutua Ghana kumn'goa mshambuliaji wa Ashanti Gold Mumuni Shafiu mwenye umri wa miaka 24

Na pengine wakaenda hata Namibia kuiwania saini ya Isaskar Gurirab anaecheza katika timu ya Life Fighters, ambayo alijiunga nayo mwaka 2018

Yanga imejipanga kufanya usajili makini ambapo inawatumia maafisa wake kuwafuatilia wachezaji wote wanaotaka kuwasajili ili kujiridhisha na uwezo wao pamoja na kuwa ni mapendekezo ya kocha Luc Eymael

Ule utaratibu wa wachezaji kuja kufanya majaribio hautakuwepo kwenye usajili ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’