Yanga haina kesi ya kujibu kwa suala la Chama - Mwanasheria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Apr 2020
Yanga haina kesi ya kujibu kwa suala la Chama - Mwanasheria

Kulingana na maoni ya Mwanasheria Dickson Mgalike, amesema haoni kama Yanga itakuwa na kesi ya kujibu kwa madai ya Simba kuhusu mchezaji wao Clatous Chama

Mgalike anasema lazima kitendo cha uvunjifu wa sheria kithibitishwe ndo kuwe na kosa

Hivyo kosa litakuwepo kama Chama au Wakala wake watathibitisha kuwa wamefanya mazungumzo na uongozi wa Yanga

Hata hivyo tayari Chama mwenyewe amekanusha kama ilivyokuwa kwa Mwakalebela kuwa hakukuwa na mazungumzo yoyote yaliyofanyika

"Ili kuwepo na kosa kuna mambo mawili lazima yafanyike, kwanza nia ovu na pili kufanya kitendo. Nia ovu ni dhamira ya mtu kwenda kufanya uharifu, na kitendo ni kile ambacho mtu anaenda kutekeleza nia yake ovu, hivi vitu lazima viende pamoja"

"Je uongozi wa Yanga au Ndg Mwakalebela walikuwa na nia ya kuzungumza na Chama? Hili ni gumu kulithibitisha isipokuwa Chama kama mchezaji au wakala wake waseme walipelekewa taarifa rasmi na uongozi wa Yanga au ndg Mwakalebela kutaka kuzumza nao"

"Pili, kitendo ni pale uongozi wa Yanga kama wamekaa na mchezaji au wakala wake wakajadiliana kuhusu mkataba, kama kuna vitu hivyo vimefanyika hapa tutasema Yanga wanayo kesi ya kujibu"

"Kwa maelezo ya mchezaji Chama na pia Mwakalebela wameeleza hakuna mazungumzo yeyote ya pande hizi mbili wamewahi kukaa na kujadili kuhusu suala la mkataba"

"Turudi kwenye kanuni, kanuni haijazungumza kama kiongozi wa timu furani akimzungumzia mchezaji wa timu nyingine kwenye vyombo vya habari na sio kwa lugha ya kejeli ndio wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo"

"Yanga hawana kesi ya kujibu na pia hakuna kosa lililotendeka, ili liwe kosa mbele ya sheria ni lazima kuwepo kwa kuvunjwa kwa sheria na kama sheria haikuvunjwa basi hapo hakuna kosa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’