Wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likipokea sakata la Makamu Mwenyekiti wa Yanga Frederick Mwakalebela, Bosi wa zamani wa timu hiyo Dk Jonas Tiboroha ameomba Simba kuelewa msamaha wake kisha akashauri.
Tiboroha amesema kauli ya Mwakalebela haikuwa kitu kizuri kwa kutamkwa na kiongozi wa hadhi yake kutokana na aliwahi kufanya kazi sehemu kubwa kuliko Yanga.
Tiboroha ambaye amewahi kuwa Katibu mkuu wa Yanga amesema kosa ambalo Mwakalebela anaonekana amefanya yapo mengi na yanafanywa na viongozi wengi na kwamba ni wakati wa kutoa elimu ya maadili kwa viongozi mbalimbali wa soka.
Kigogo huyo ambaye aligombea nafasi ya Mwenyekiti katika uchaguzi wa Yanga uliopita amesema kuna haja ya TFF kufanya mchakato wa kuwaandalia semina ya kuwakumbusha wadau wake juu ya miiko ya uongozi.
Aidha kigogo huyo amesema amesikia kwamba Mwakalebela ameomba radhi na kwamba haitakuwa hatua mbaya kwa Simba kumsamehe kwani makosa hayo yanafanyika sana kwa nyakati tofauti baina ya viongozi hao.
Ameongeza kwamba endapo Simba watamchukulia hatua Mwakalebela hatua hiyo inaweza kujenga chuki baina ya viongozi wa klabu hizo kongwe mbili kupitia makosa yanayoweza kujitokeza kiungozi