Inalezwa mshambuliaji wa Namungo Fc Reliants Lusajo amegoma kuongeza mkataba mpya na timu hiyo hadi msimu utakapomalizika
Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye rada za klabu ya Yanga inayomuwania kumjumuisha kwenye kikosi chake cha msimu ujao
Mwenyekiti wa Namungo Fc Hassan Zidadu ameeleza kuwa wameanza mazungumzo na nyota wao watatu ambao wanawindwa na vilabu vya Yanga, Simba na Azam Fc
Hata hivyo amesema wakati mazungumzo na Lucas Kikoti na Bigirimana Blaise yakienda vizuri, Lusajo yeye ametaka mchakato wa mkataba mpya uanze mwishoni mwa msimu
Lusajo ambaye ameifungia Namungo Fc mabao 11 msimu huu anatajwa kukaribia kutua Jangwani kwa mara ya pili, kwani aliwahi kupita mitaa hiyo mwaka 2013
Lusajo amekuwa katika kiwango bora tangu alipojiunga na Namungo ambapo msimu uliopita alichangia kuipandisha timu hiyo daraja baada ya kuifungia mabao 15
Ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza msimu uliopita