Sare ni matokeo 'rafiki' kwa Pluijm na Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2017
Sare ni matokeo 'rafiki' kwa Pluijm na Lwandamina
Mchezo dhidi ya Singida United ulikuwa mgumu kama ilivyotarajiwa. Matokeo ya sare ni matokeo 'rafiki' kwa timu zote.

Singida United ilikamia mchezo huo na walikuwa na sababu ya kukamia.

Ikumbukwe mchezo huo umeweka historia kwa klabu ya Singida United kucheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya miaka 5 kupita ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2012.

Katika mechi za raundi 8 zilizopita msimu huu Singida United ilikuwa ikitumia uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo Namfua ulikuwa unafanyiwa marekebisho kabla ya Bodi ya ligi kuupitisha rasmi uwanja huo mapema mwezi uliopita.

Hivyo Singida United ilitamani sana kupata ushindi dhidi ya mabingwa ili kuiandika Historia yao vizuri.

Hans van Pluijm na George Lwandamina ni sababu nyingine ya mchezo huo kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Inafahamika Pluijm ndiye aliyempisha Lwandamina yeye akipewa cheo cha Ukurugenzi wa Ufundi, cheo ambacho kilifutwa na Pluijm kupoteza ajira baada ya Yanga kukumbwa na 'ukata'.

Pluijm ni 'master' wa soka la kushambulia hilo halina ubishi. Singida United ni moja ya timu bora kabisa msimu huu.

Timu hii iko katika daraja sawa sawa na Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa katika mbio za ubingwa.

Ni dhahiri Pluijm leo alihitaji zaidi ushindi ili apeleke 'salamu' kwa viongozi wa Yanga.

Hata hivyo Lwandamina ni 'master' wa soka la kujilinda. Yanga msimu huu inajivunia safu imara ya ulinzi.

Mfumo unaotumiwa na Lwandamina wa kujilinda pamoja na kushambulia kwa pamoja umeifanya Yanga kuwa timu ngumu kufungika.

Msimu huu upo uwezekano wa kutopoteza mchezo kama wachezaji wataendelea kujituma kwenye ulinzi kama wanavyofanya sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’