GSM wanavyorudisha heshima ya Yanga kwenye usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2020
GSM wanavyorudisha heshima ya Yanga kwenye usajili

Kwa misimu mitatu iliyopita klabu ya Simba ilitawala zaidi kwenye soko la usajili, fedha za Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' zikiwapa kiburi mabingwa hao watetezi ligi kuu

Kabla ya hapo ni Yanga iliyokuwa ikisumbua wakati wa Mwenyekiti Yusufu Manji ambaye alitumia mamilioni kukisuka kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

Ukiangalia usajili uliofanywa na Simba ndani ya misimu mitatu iliyopita, nyota wengi waliokuwa wakinyemelewa na Yanga walisajiliwa kibabe na timu hiyo kutokana na jeuri ya fedha

Utaratibu huo ulianza kushika mizizi kwani klabu hiyo pia ilisajili moja kwa moja wachezaji kutoka klabu ya Yanga

Ni msimu huu huu mwanzoni Simba ilisajili nyota watatu muhimu wa Yanga Beno Kakolanya, Gadiel Michael na Ibrahim Ajib aliyekuwa kipenzi cha mashabiki

Usajili wa Gadiel ulifanyika siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa, nyota huyo akirudisha mkataba wa Yanga aliokuwa amekabidhiwa kabla ya kwenda kushiriki michuano ya Afcon nchini Misri

Lakini tangu GSM waanze kuidhamini Yanga mwezi Januari, heshima ya mabingwa hao wa kihistoria kwenye usajili imeanza kurejea

GSM waliingia wakati ambao nyota wengi wakigeni walikuwa wakivunja mikataba yao baada ya kukosa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu

GSM walifanikiwa kumrejesha beki Lamine Moro ambaye alikuwa tayari amerejea kwao Ghana

Lakini pia wakaweza kuwasajili Haruna Niyonzima, Barnard Morrison, Adeyum Saleh, Erick Kabamba na Yikpe Gnamien

GSM wameendelea kuipa Yanga heshima baada ya kuzima jaribio la klabu ya Simba kuwasajili Morrison na Papy Tshishimbi ambao mikataba yao ilikuwa ikielekea ukingoni

Pengine wachezaji hao ndio wameziiingiza timu hizo kwenye vita ya usajili inayoonekana sasa

Kwani GSM wamepanga kulipa kisasi kwa kusajili nyota wa Simba ambao mikataba yao iko mbioni kumalizika

Nyota wanaotajwa kuwa kwenye rada za GSM ni pamoja na Clatous Chama ambaye klabu ya Simba kupitia msemaji wao wametishia kwenda kushitaki FIFA wakiituhumu Yanga kuanza mazungumzo mapema na nyota huyo ambaye wanadai mkataba wake ni zaidi ya miezi sita

Lakini GSM wamekwenda mbali zaidi wakiitaka Simba iweke hadharani dau wanalotaka kwa ajili ya nyota huyo

Nyota wengine wanaohusishwa kwenye mpango wa GSM ni mawinga Deo Kanda na Hassan Dilunga ambao mikataba yao iko mbioni kumalizika

Aidha kwa Kanda, Yanga inapaswa kumalizana na TP Mazembe ambayo ndio inayommiliki mchezaji huyo

Kwa kasi waliyorejea nayo GSM, ni wazi imepeleka hofu pale Msimbazi kwani wanaonekana kuwa na shauku ya kurejesha heshima ya Yanga kwa soka la Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’