Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amedai kuwa hataacha kuisema na kuishambulia klabu ya Yanga kwa kila namna kwa kuwa ndio kazi aliyoletwa kuifanya duniani
Akihojiwa na Wasafi FM mapema leo, Manara amesema ameletwa duniani kwa kazi mbili tu, kufanya ibada na kuishughulikia Yanga
"Nililetwa duniani kwa ajili ya vitu viwili tu yaani Kumuabudu Mungu na kuwashughulikia Yanga," kauli ya Haji Manara ambaye baba yake mzazi Sunday Manara 'computer' alicheza kwa mafanikio klabu ya Yanga
Sunday ni 'legendary' wa klabu ya Yanga, amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ya klabu ya Yanga
Kuna wakati Mzee Manara aliwaambia Wayanga wasitishwe na Mwanawe (Haji) kwani wao ndio waliomlea
ADVERTISE HERE