Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amefichua kuwa timu hiyo inaweza kumuwania kiungo wa Simba Clatous Chama
Mwakalebela amesema wanafahamu mkataba wa Chama na Simba umebakisha chini ya miezi sita hivyo wanaruhusiwa kuzungumza nae
Aidha Mwakalebela ameongeza kuwa sio Chama tu wanayemtaka, yuko mchezaji mwingine ambaye wana uhakika watampata
"Chama ni mchezaji mzuri sana na hakuna mwalimu asiyependa kufanya nae kazi," Mwakalebela aliiambia eFM
"Najua kuwa Chama amebakisha kandarasi ya miezi 6 na ndicho wengi tunachokijua mpaka sasa na nasema hivi sio Chama tu pia kuna mwingine tunamsaka pale na tutampata tu"
Ni kama Yanga imeamua kuwavuruga watani zao hasa baada ya Simba kujaribu kuwasajili Benard Morrison na Papy Tshishimbi ambao hata hivyo Yanga imefanikiwa kuwaongeza mikataba