FT : Singida United 0-0 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2017
FT : Singida United 0-0 Yanga
Mchezo wa ligi ya Vodacom mzunguuko wa tisa kati ya Singida United dhidi ya mabingwa watetezi Yanga umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Mchezo huo uliotawaliwa kwa kiasi kikubwa na wenyeji Singida United umepigwa katika uwanja wa Namfua ambao umezinduliwa rasmi leo.

Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi kwenye dakika 10 za mwanzoni kabla Singida United haijazinduka na kupeleka mashambulizi langoni mwa Yanga.

Licha ya mashambulizi ya hapa na pale kutoka kila timu, hakuna timu iliyoweza kuzifumania nyavu za timu pinzani ingawa Singida United walicheza vizuri zaidi kuliko Yanga kwenye kipindi cha pili.

Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga Hans van Pluijm ilipeleka mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga katika kipindi cha pili hata hivyo kazi nzuri iliyofanywa na mlinda lango Youthe Rostand iliiwezesha Yanga kuondoka ugenini na alama moja muhimu



Kwenye dakika ya 54 wachezaji wa Singida United walitaka kuzua tafrani baada ya kumvaa mwamuzi wakitaka wapewe bao kutoka mpira wa kichwa uliopigwa na Michelle kisha kutinga wavuni kupitia tundu la nyavu zilizotoboka pembeni.

Mpira huo ulipitia nje kisha kutinga wavuni.



Yanga ilifanya mabadiliko ya wachezaji wawili ambapo kwenye dakika ya 60 Geofrey Mwashiuya alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Emanuel Martini huku Pato Ngonyani akitoka kwenye dakika za lala salama nafasi yake ikichukuliwa na Raphael Daudi.

Matokeo ya suluhu yameifanya Yanga ifikishe alama 17.

Azam FC iko kileleni baada ya kufikisha alama 19 kutokana na ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Aidha Simba inayocheza kesho Jumapili dhidi ya Mbeya City inaweza kurejea kileleni kama itashinda.

Michezo mingine mitatu imemalizika kwa sare pia.

Ndanda 0-0 Mtibwa
kagera 1-1 prisons
Njombe 0-0 Mbao
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’