Hiyo wiki ya Mwananchi ya mwaka huu usipime

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2020
Hiyo wiki ya Mwananchi ya mwaka huu usipime

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema shamrashamra za wiki ya Mwananchi mwaka huu zitakuwa za aina yake

Sherehe za mwaka huu zitakuwa za pili kwa Yanga iliyoanzisha utaratibu huo kwa mafanikio mwaka uliopita

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amefichua kuwa shamrashamra za mwaka huu watazifanya katika 'level' nyingine kabisa kwani wataandaa mambo mazuri zaidi

"Huu utakuwa mwaka wetu wa pili kuandaa wiki ya Mwananchi, tutafanya jambo kubwa zaidi. Kwa sasa hatutazungumza mengi, tuombe mungu atuepushe na hii changamoto ya corona. Lakini sipati picha kilele cha mwaka huu kitakuwaje, itakuwa zaidi ya mwaka jana.."

Nugaz alisherehesha tukio la kwanza la aina hiyo ambalo lilifanyika uwanja wa Taifa na kushuhudia mashabiki wa Yanga wakifurika kwa wingi

Kwa michakato ya maboresho ya kikosi inayoendelea sasa, ni wazi timu ya mwaka huu itawavuta mashabiki wengi zaidi uwanjani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’